Tuesday, May 29, 2012

kuruka muhimu jamani

Ratifa Abdallah akijaribu Bajaj aliyokabidhiwa na Kaimu Mnikulu kwa niaba ya Rais Kikwete.

Irine Malekela naye akijaribu bajaj yake baada ya kukabidhiwa.
Serikali yasitisha tiba ya Loliondo

Na Waandishi Wetu

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Shirima kuzuia haraka matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo.

Dk Mponda alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua matumizi ya Bajaji kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa.

MCHUNGAJI Mstaafu Ambilikile Mwasapile akiendelea na kazi ya kutoa dawa
Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumzuia mchungaji huyo kuendelea na utoaji wa dawa mpaka serikali itakapojiridhisha na hali ya usalama pamoja na uwezo wa dawa hiyo.
“Kutokana na hali halisi ya usalama wa kiafya kwa sasa katika eneo hilo, kuna hatari ya kuwepo kwa milipuko ya magonjwa kwa kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka,” alisema Dk Mponda.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymund Mushi alisema hajapata taarifa yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya Wizara ya Afya... "

Hadi jioni hii mpaka ninatoka ofisini sijapata taarifa yoyote kuhusiana na uamuzi huo."Baadhi ya wananchi waliohojiwa kuhusiana na hatua hiyo ya Serikali walisema badala ya kuchukua hatua hiyo, ilipaswa kusimamia mchakato mzima wa utoaji wa dawa hiyo kwa kuhakikisha kwamba inatolewa katika mazingira mazuri na kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinapatikana kijijini hapo ikiwa ni pamoja na kuwabana wamiliki wa magari kupunguza nauli na kukarabati barabara.

Mkazi wa Karatu, Reurent Bortha, alisema anashangazwa na serikali kuibuka sasa wakati mchungaji huyo alianza kutoa dawa hiyo tangu Agosti mwaka jana... "Tunaiomba serikali kusaidia upatikanaji huduma muhimu kama mahema na kukarabati barabara na siyo sasa kuibuka na kusema dawa haijafanyiwa utafiti."

Bortha ambaye amedai kwamba ndugu zake wamepona maradhi mbalimbali kutokana na dawa ya mchungaji huyo, alisema serikali imechelewa kufanya utafiti wa kuthibitisha dawa hiyo kitaalamu na inachopaswa kufanya ni kuweka mazingira bora ya utolewaji wake.Mwananchi mwingine, Peter Ngoi alisema kama serikali inatilia shaka dawa hiyo, inapaswa kuwafuata watu waliokunywa na kupona na siyo kuhangaika kuipima na kuichunguza... "Hawa watu wa Serikali ni wa ajabu hawajazungumza na sisi wagonjwa wanakaa Dar es Salaam na kutangaza kusitisha dawa."

Dk Mponda alisema serikali ilishaanza kuchukua hatua za awali ikiwepo ya kupeleka wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ambao alidai kuwa wamewasili eneo hilo tangu Jumanne iliyopita na kuanza kufanya uchunguzi.

Alisema utaratibu wa kisheria wa utoaji wa dawa unamtaka atakayegundua dawa ya aina yoyote anatakiwa kufuata taratibu zilizopo ikiwemo kuthibitishwa na TDFA ili kuangalia ubora na madhara yake kwa watumiaji.“Sheria zipo, tatizo lililopo ni katika usimamiaji. Hata hivyo, inachukua muda mpaka utaratibu wa kuithibitisha dawa kama inafaa au haifai kwa matumizi ya kutibu magonjwa ya binadamu," alisema Dk Mponda.

Akizungumza katika uzinduzi wa matumizi ya pikipiki hizo, Dk Mponda alisema zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya kubebea wagonjwa. Alisema katika awamu ya kwanza, Serikali imenunua pikipiki 400 maalumu kwa ajili ya kubebea wagonjwa zenye thamani ya dola za Marekani 5,900 kila moja.

Waziri huyo alisema pikipiki hizo zitagawiwa katika mikoa yenye matatizo ya usafiri hasa maeneo yenye milima ikiwamo Rukwa, Mbeya, Pwani, Morogoro na Dodoma.Dk Mponda alisema pikipiki hizo zimekuwa usafiri wa uhakika kwa wagonjwa katika nchi za Afrika ya Kusini, Sudani, Kenya na Senegal, Malawi, Ethiopia na Guinea.





Mchuchuma kufua umeme Megawati 600

Na Bazil Makungu Ludewa
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madili imeshangazwa kusikia kuwa Makaa ya mawe ya Mchuchuma peke yake yanaweza kufua umeme wa uhakika nchini kwa muda wa miaka mia moja na sitini (160) na kuondokana na adha ya nishati hiyo inayoendelea kulisumbua Taifa kwa mgawo kila kuchapo.

Dr Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mbunge msitaafu wa jimbo la kwera Mkoani Rukwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi katika Shirika la Taifa la Maendeleo nchini (NDC) aliyasemahayo jana kwenye kamati hiyo ya Bunge ilipotembelea kujionea hali halisi iliyopo Mchuchuma, Ketawaka na Liganga Ludewa.

Mzindakaya aliiambia kamati hiyo kuwa makaa yam awe ya Mchuchuma na Liganga yamecheleweshwa na watoa maamuzi kwa kuingiza siasa kwenye utendaji kwa kuwa tegemezi kwa watu wan je.Tulikuwa tunafanya makosa makubwa kutegemea wageni kwa kila kitu badala ya kufanya sisi wenyewe, aliongeza.

“mimi ningekuwa mwamuzi mwenyewe bila kuingiliwa na mtu Mchuchuma ingeanza hata kesho kwa sababu ndani ya kichwa change hakuna harufu ya epa wala Richmond.na mambo hayo ndiyo yametawala ndani ya vichwa vya viongozi waliowengi na ndiyo maana kila mtu anahofu hakuna aliye tayari kuthubutu,” alisikitika Mzindakaya

Akijibu swali la Zito Kabwe Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini aliyetaka kujua kwa kipindi chote viongozi waliotangulia akiwemo yeye mzindakaya walikuwa wapi mpaka Taifa linaingia kwenye giza. Mzindakaya alisema tulicheleweshwa na watoa maamuzi waoga.

Alisema mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Ketewaka na Chuma cha Liganga tutahakikisha mali hiyo inalindwa kwa maslahi ya umma,hatutaruhusu mwekezaji yeyote kupata kiasi kikubwa huku Serikali ikiambulia sehemu ndogo ya pato linalopatikana katika miradi mingi hapa nchini.ni lazima tupate asilimia hamsini kwa hamsini kwa sababu sisi ndiyo wenye raslimali tofauti na awali ambapo tulikuwa tukiibiwa kwa visingizio vya mtaji na teknolojia.

Mwenyekiti huyo wa bodi aliiambia kamati ya Bunge kuwa Tanzania tumekuwa tukinyonywa na wawekezaji kwa sababu hatujui kilichopo katika migodi yetu alisema zamani waingereza walitudanganya kuwa Mchuchuma ilikuwa na tani m.40 lakini tulipofanya wenyewe kwa ktumia wataalamu wa ndani tuligundua kuwa tunazo zaidi ya tani 1.2 bilioni.

Bila Mkaa wa Mawe wa Mchuchuma na Ketawaka hakuna Liganga kwa hiyo tuliweka masharti kwa wawekezaji kuwa atakayetaka kuwekeza Liganga lazima lazima awekeze na Mchuchuma kwa sababu miradi hii inategemeana, na katika mrdi huu tulishindanisha makampuni kumi na nne.

Akitoa maelekezo na ushauri kwa NDC Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Bw Zito Kabwe alisema kuwa huu ndiyo mwisho wa porojo lazima sasa wananchi waone kweli Liganga na Mchuchuma imeanza kutoa matunda na mawasiliano yafanywe kila mara kati ya kamati hiyo na NDC.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mkomang’ombe kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa kamati hii imekuja kuhakisha maendeleo yanapatikana ndani ya Ludewa na Taifa,yale maneno ya michakato yamekwisha tumeshatoa maelekezo kwa wahusika.

Tuesday, March 8, 2011

MAELFU YA WATANZANIA WAENDELEA KUMIMINIKA LOLIONDO KWA MCHUNGAJI

Hii ni sehemu ya foleni ya magari inayokadiliwa kuwa na urefu wa Kilomita kumi, ikielekea Kijiji cha Samange Kata ya Digodigo Wilaya ya Ngorongoro, kwa ajili ya kupatiwa dawa ya jero (500) inayodaiwa kutibu magonjwa matano sugu likiwamo la Ukimwi pamoja

Mamia ya magari yanaidi kuja loliondo
Hapa ni baadhi ya wananchi waliofanikiwa kufika wakiwa katika foleni kwa ajili ya kusubiri kunywa dawa hiyo na kumuona huyo Babu, ambaye sasa amegeuka kuwa moja ya kivutio.

Sunday, March 6, 2011

MPAMBANO WA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA


VIKOSI VYA SIMBA (JUU) NA YANGA (CHINI)



WACHEZAJI WA SIMBA NAO WAKIPONGEZANA BAADA YA KUSAWAZISHA BAO
MASHABIKI WA SIMBA WAKISHANGILIA BAADA YA TIMU KUSAWAZISHA BAO

AFISA HABARI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF), KUSHOTO, BW. BONIFACE WAMBURA AKIFUATILIA MPAMBANO HUO ULIOCHEZWA MWISHONI MWA JUMA KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

Wednesday, February 16, 2011

Jane Mihanji (kulia) na mimi tukipiga story wakati wa Bonanza la Waandishi wa Habari lililoandaliwa na Kampuni ya Airtel liliofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mdau Balegeya akitafakari mambo yalivykuwa yakijiri katika viwanja hivyo kama anavyoonekana akiwa katika pozi kali la picha.

Wadau Dada Winn na kaka Mohamed, wakishangaa jambo katika viwanja hivyo, walikuwa wakipiga story hamad wakastukio jambo lililowaacha mdomo wazi ambalo lilikuwa likifanywa na mmoja wa wanahabri amabye hayupo pichani.


Kadaaaa Khadija akijaribu kuzirudi ngoma za msondo zilizokuwa zikipigwa viwanjani hapo kama anavyoonekana kulia kwa huyo mdada anaye dansi naye.

Wadau kutoka kushoto Ester Mvungi, Rhodar Kangero na Selina Wilsoni, walikuwa miongoni mwa wanahabari kutoka Uhuru Publictaions Ltd, waliojitosa katika bonanza hilo.


Msondo waliwakuna wengi, mmoja wapo ni brother Mohamed kama anavyoonekana akilisakata rhumba la Msondo.


Katika bonanza hilo, kulishindaniwa michezo mbalimbali, UPL hawakubaki nyuma, walijitosa katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo walifanikiwa kulitwaa kombe kama wanavyoonekana wakijidai na kombe hilo!!!!!!!




Rais Jakaya Kikwete, na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman, wakisoma dua wakati wa sala ya mwili wa aliyekuwa dereva wa Ikulu, marehemu Ramadhani Said, aloyefariki kwa ajali ya gari, eneo la Ruvu Darajani, Dar es Salaam.
Hili ndilo Baraza Kivuri la Mawaziri kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni, kama lilivyotangwazwa hivi karibuni na Kiongozi Mkuu wa Kambi hiyo, Mbunge wa Hai CHADEMA, Freeman Mbowe.
RAIS Jakaya Kikwete akimpa pole mtoto Brenda Boniface(4) aliyelazwa katika Hospitali ya shirika la Elimu Kibaha mkoa wa Pwani kwa kuugua malaria, baada ya kufungua jengo la Mama na Mtoto lililojengwa na Taasisi ya Korea Rotary Internationa katika hospitali hiyo, leo.Kulia ni mama wa mtoto huyo,Tiasaeli Palangyo.(Picha na Freddy Maro)

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto, akieleza yalipofikia maandalizi ya Bonanza hilo, leo, kwenye Ofisi za Kampuni ya Bia Tanzaania (TBL), Ilala, mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mweneyekiti wa TASWA, Maulidi Kitenge na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Amir Mhando na wapili kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi, ambaye alithibitisha TBL kudhamini bonanza hilo.


Vijana wapewe matumaini kuepusha vurugu


Na Mwadishi Maalum, New York
TANZANIA imeshauri kwamba ili kuliepusha Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla na vitendo vya uvunjifu wa amani, ni vema vijana wakapewa matumaini ya kuwa na maisha bora.Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, wakati Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipokutana mwishoni mwa wiki, kujadili uhusiano uliopo kati ya usalama na maendeleo.Katika hali ambayo wanadiplomasia waliiona si ya kawaida na kuibua hisia mbalimbali, Baraza hilo lilitenga siku nzima ya ijumaa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu udhibiti wa amani na usalama. na uhusiano uliopo kati ya suala zima la usalama na maendeleo.Mada hiyo ilipendekezwa na Brazil, nchi ambayo kwa mwezi huu wa February ndiyo Rais wa Baraza hilo.Mwakilishi huyo wa Tanzania, amewaeleza washiriki wa mjadala huo uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ukiwashirisha pia wawakilishi wa Bank ya Dunia, na baadhi ya mawaziri kwamba,“ Ni jambo lililodhahiri kuwa kukata tamaa, kunyimwa fursa, na ufukara na hasa miongoni mwa vijana, ni chachu tosha ya tishio kwa amani na usalama katika nchi moja moja na dunia kwa ujumla”Akasema vitendo vya uhalifu kama vile biashara ya dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu , uharamia, ugadi na uhamiaji haramu ni matokeo ya umaskini.Balozi Sefue amebainisha katika hoja yake kwamba, suala la usalama ni la msingi sana kwa maendeleo, na maendeleo kimsingi ni usalama na Baraza hilo haliwezi kulikwepa hilo.Anasema “Kwa kuwapa matumaini vijana wa Afrika, matumaini ya kuwa na maisha bora huko mbeleni, kutasaidia sana kupunguza shinikizo la kuwapo kwa vitendo vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani, uhalifu na migogoro”.Akaongeza kuwa watu wanatakiwa kushirikishwa katika suala zima la usalama na maendeleo yao, katika njia sahihi na bora itakayoimarisha amani na kuibua mazingira sahihi ya utawala bora, na kuheshimu haki za binadamu.Awali akifungua mjadala huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, hakusita kueleza bayana kwamba, matukio kadha ambayo yamekuwa yakiendelea katika baadhi ya nchi katika siku za hivi karibuni yalikuwa ujumbe mzito kuwa hali ya mambo si shwari.Anasema Ban Ki Moon. “ Matukio ya hivi karibuni duniani, yanabeba ujumbe mzito kwamba, kunahitajio la kuwapo kwa utulivu wa kisasa unaojikita katika amani, fursa sawa, uhakika wa maisha bora na matakwa ya wale wanaotawaliwa”.Akasema amani, usalama na maendeleo ni mambo yanayohusiana au kutegemeana. Na ushahidi unaonyesha wazi kuwa katika kipindi cha miaka 20, nchi nchi tisa kati ya kumi ambazo viwango vya maendeleo viko chini zimekubwa na migogoro.Aidha akasema, nchi ambazo wananchi wake hawana fursa sawa, huku taasisi zake zikiwa dhaifu ziko katika hatari kubwa ya kutumbukia katika migogoro.“ Mgawanyo usio sawa wa raslimali, ukosefu wa nafasi za ajira, fursa na uhuru na hasa kwa idadi kubwa ya vijana kunaweza kuwa chimbuko kubwa la uvinjifu wa amani” anasisitiza Ban Ki Moon.Akawaeleza wajumbe wa mjadala huo kwamba, kama ukosefu wa maendeleo unaweza kuwasha moto wa machafuko, halikadharika kuwapo kwa uchumi imara na maendeleo ya kijamii, kunaweza kupunguza mlipuko wa mioto hiyo na hivyo kuwapo kwa hali ya amani.Karibu wajumbe wote waliochangia mjadala huo, Tanzania ikiwamo, licha ya kukubaliana kwamba, usalama na maedeleo ni mambo yanayowiana, lakini walitahadharisha kwamba Baraza hilo halikuwa na dhamana ya kulijadili na lilikuwa linafanya kazi ya vyombo vingine vya Umoja wa Mataifa kama vile Baraza Kuu la Umoja huo.Balozi wa Misri katika Umoja wa mataifa, yeye hakusita kabisa kuelezea hisia zake pale aliposema huenda mchakato wa mageuzi yaliyokuwa yakiendelea nchi mwake ndiyo yaliyopelekea kuwapo kwa mjadala huo.Akasema kuwa ingawa anakubaliana na ajenda hiyo, lakini alikuwa anatoa tahadhari kuwa isingekuwa busara wala haki kuyahusisha mageuzi ya kisiasa nchi mwake na mjadala huo.


MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pfofesa Rwekaza Mukandala, hicho na Chuo cha Biashara cha Milpak cha Afrika Kusini, leo katika Hoteli ya Movenpic mjini Dar es Salaam. Wengine ni Dk. Riwa Colman wa Tanzania Institute Of Bankers na Mkurugenzi wa Teknolojia ya mawasiliano wa CRDB, Elyas Mtengwa.

CHUO Cha Biashara cha Milpak cha Afrika Kusini kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kimeingia mkataba wa kufundisha masomo kwa njia ya mtandao kwa wafanyakazi wa Taasisi 11 za Benki hapa nchini, ikiwemo CRDB. Pichani, Mkurugenzi Mkuu wa Milpaki, Julian Van-Der-Westhusein, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala, wakitia saini mkataba wa uendeshwa wa masomo hayo,leo. hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam.


TASNESCO wahaha na mgawo wa umeme


Na Lilian Timbuka

SHIRIKA la Umeme nchini, Tanesco, sasa limenunua mafuta ya kuendeshea mtambo wa umeme wa IPTL uliopo, Tegeta, Dar es Salaam, ili kuzalisha megawati 80 kwa siku, ikiwa ni moja ya hatua zake kujaribu kupambana na mgawo wa umeme ambao shirika hilo limekiri kuwa unalipunguzia heshima kwa umma.
Akizungumza na waandshi wa habari , kwenye makao makuu ya Tanesco, Ubungo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Injinia, Felchesmi Mramba,(Pichani), alisema, mafuta yameshanunuliwa na yameanza kuwasili IPTL, ili kuzalisha kiasi hicho cha megawati za umeme kwa siku.
"Hii itapunguza mgawo wa umeme kwa sasa kwa megawati zipatazo 70", alisema Injinia huyo ambaye alifuatana na Meneja Uhusiano wa Shiruika hilo, Badra Masoudi (kulia) na kuongeza "tunatarajia kwamba msimu wa mvua za masika utaanza punde, na hii itafanya uzalishaji wa umeme katika mitambo ya maji kuongezeka na hivyo kuliondoa tatizo hilo kwa sasa.
"Pia Shiruka linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mit ambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani unaotarajiwa", akasema Injinia Mramba.
Akasema, uongozi wa Tanesco unawaomba radhi sanaaaa, wananchi kutokana na usumbufu mkubwa unaotokana na adha ya mgawo huo wa umeme na pia Shirika linawasihi wananchi kushirikiana na shirika hilo, na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha upungufu wa umeme.
"Tunaahidi kwamba tutafanya kila jitihada kurekebisha mapungufu balimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili la mgawo hasa kudhibiti matukio ya dharura yanayofaya ratiba zisifuatwe kama zilivyopangwa", akamaliza..
Na Mwandishi Maalum. New York

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, ambaye ni Mwenyekiti wa Timu ya watu watatu iliyoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, kuangalia mchakato wa maandalizi na hatimaye upigaji kura ya maoni katika Sudan ya Kusini. Ameliambia Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa matokeo ya kura hiyo ni ya haki, huru na kuaminika.

Rais Mstaafu Mkapa, ameyasema hayo siku ya jumatatu wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa yake mbele ya Baraza hilo, ikiwa ni siku mbili zimepita tangu kutangazwa rasmi matokeo ya kura hiyo yaliyoonyesha, kuwa asilimia 98.83 ya wananchi waliopiga kura wameamua kujitenga na kuwa na taifa lao.

“ Timu yetu inapenda kuhitimisha kwamba matokeo ya kura hiyo ya maoni yameonyesha matakwa ya wananchi wa Sudan ya Kusini, mchakato mzima wa upigaji wa kura ulikuwa wa uhuru, haki na wa kuaminika”. Anasema Mkapa. Akasema kukamilika kwa zoezi hilo ni moja ya hatua muhimu sana kuelekea upatikanaji wa amani ya kudumu.

Baada ya matokeo ya mwisho ya kura hiyo kutangazwa na baada ya pande zote mbili kuridhia na kuyakubali, huku Jumuia ya Kimataifa ikiyaridhia, Taifa huru la Sudan ya Kusini litakaribishwa rasmi katika Jumuia ya Kimataifa Julai 9 mwaka huu.

Mkapa ambaye timu yake ilitembelea Sudan ya Kusini mara tano katika kipindi cha kuelekea upigaji wa kura hiyo. Amelieleza Baraza hilo kwamba, katika kutathimini mchakato huo wote, timu yake ilizingatia misingi yote iliyoainishwa katika Sheria ya Kura ya Maoni ya Sudan ya Kusini. Na kwamba Timu imejiridhisha kuwa zoezi lilifanyika katika mazingira ya uwazi wa hali ya juu.

Akaendelea kusema kuwa asasi zisizo za kiserikali nazo zilishiriki kwa ukamilifu na kwamba kauli zilizotolewa na viongozi wa juu wa serikali pande zote mbili za Kaskazini na Kusini zinatia matumaini.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Timu hiyo, anasema kumekuwapo na kusuasua kwa utekelezaji wa masuala ya usalama baada ya upigaji wa kura, pamoja na vitendo vya hujuma ingawa kwa maoni ya timu hujuma hizo hazikuathiri zoezi la upigaji wa kura.
Akatumia nafasi hiyo kuwapongeza Rais Omar Bashir na Makamu wa Kwanza wa Rais Slava Kiir Mayardit kwa kuonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa wa kuhakikisha kwamba hatua muhimu kuelekea amani ya kudumi imefikiwa.
Hata hiyvo ametahadharisha kwamba kazi bado ni kubwa kwa pande zote mbili zinazohusika na mkataba wa amani wa kudumu. Na akatoa wito wa kumalizia vipengele vilivyobaki huku akisisitiza umuhimu wa kuwapo kwa ulinzi wa uhakika kwa wananchi wa Sudani bila ya kujali kama ni wa Kusini au wa Kaskazini.

Pamoja na Rais Mkapa kuwasilisha taarifa yake mbele ya Baraza hilo, wengine waliowasilisha taarifa ni pamoja na Rais mstaafu Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini aliyeongoza jopo la watu mashuhuri kwa niaba ya Umoja wa Afrika, taarifa yake ilisomwa na Balozi Mhmoud Kane, na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini Bw. Haile Menkerios.
Kwa upande wake baada ya kuzipokea taarifa hizo, ambazo zilifuatiwa na matamko mbalimbali yaliyotolewa na wajumbe 15 wa Baraza Kuu la Usalama. Baraza limeyapokea na kuridhia matokeo ya mwisho ya kura hiyo ya maoni.
Aidha Baraza likawapongeza Rais Omar Al Bashiri na Makamu wa Kwanza wa Rais Salva Kiir Mayardi kwa kuyakubali matokeo ya kura hiyo.
Baraza pia, limewapongeza na kuwashukuru, Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na timu yake, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na timu yake, Mwakilishi Maalum wa Katibu wa UM Bw. Menkerio, Umoja wa Afrika na Jumuia ya Kimataifa kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanikisha upigaji wa kura na matokeo yake.

Akisoma Tamko la Baraza hilo, Rais Baraza kwa mwezi huu, ambaye ni Brazil, Balozi Maria Luiza Ribeiro. Amesema Baraza linatoa wito kwa Jumuia ya Kimataifa kuwasaidia kwa hali na mali wananchi wa Sudan ya Kusini katika kuijenga nchi yao. Pamoja na kulitambua Taifa hilo ifikapo Julai

Baraza Kuu linasisitiza katika tamko lake kwamba ili amani ya kudumu na usalama iwe dhahiri katika Sudan na eneo lote kwa ujumla, ni muhimu vipengele vilivyobaki katika Mkataba wa Kudumu wa Amani vikatekelezwa haraka.
“ Wajumbe wa Baraza linazihimiza pande zote za Mkataba wa Amani kukutana haraka na kukubaliana kuhusu eneo lenye mgogoro la Abyei, suala la mipaka, mpangilio wa masuala ya usalama, uraia, deni la kitaifa, sarafu, mali na ushirikiano katika utajiri na maliasili” anasema Balozi Maria Luiza Riberio.
Aidha Baraza Kuu la Usalama limewataka na kuwahimiza viongozi wa Sudan ya Kaskazini na Kusini kuendelea na moyo na utashi ambao wamekwisha kuuonyesha na kwamba Jumuia ya Kimataifa ipo pamoja nao.


MWENYEKITI wa timu ya watu watatu iliyoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kuangalia mchakato wa kura ya maoni Sudan Kusini, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akiwasilisha taarifa yake mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, jana, Ijumatano, kuhsu mchakato huo na matokeo ya kura. maataokeo ya mwsiho ya kura hiyo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, yameonyesha kuwa asilimia 898.83 ya waliopiga kura wameafiki Sudani Kusini ijitenge na kuwa taifa jipya.

Wednesday, February 9, 2011

Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa na mwalimu wao, kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Uhuru Publications Ltd, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, leo.
Msaidizi wa Mhariri wa Mzalendo, Kulwa Magwa (kushoto), akimtambulisha Msanifu wa Uhuru, Lilian Timbuka (kushoto), kwa wanafunzi hao.

Magwa akitoa maelezo ya utayarishaji wa gazeti wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, yanayochapishwa na Uhuru Publications Ltd (UPL), hapa wapo katika chumba chumba cha habari.


KIKAO CHA PILI CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KIKIENDELEA LEO MJINI DODOMA



Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, wakimsubiri kwa mabango kama hili, Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa, kabla ya kufika chuoni hapo kuwasili kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu nyongeza ya sh. 10,000 wanayotaka waongezwe kwenye fedha za kujikimu.

Mwanafunzi akiwa amejifunga utepe wa polisi baada ya kuung'oa eneo ulikokuwa umewekwa na polisi kwa ajili ya usalama.

No comments:

Post a Comment